1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara. Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake. 2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako. Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani. Kama kuna mtu kakwambia, Flani njoo kesho nikulipe deni lako Basi wewe usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na ww umeahidiwa 3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia. Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki. 4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa. Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo. Maarifa ndio mtaji wa kwanza. Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema, "Omba ndoano, usiombe samaki" 5. Usitunze mbegu badala ya
The main aim of students forums blog to provide the fact and accurate information concerning with students in order to be aware.