Skip to main content

KANUNI MUHIMU UNAZOPASWA KUZIFAMU KUHUSU PESA



1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara. Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.

2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako. Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani.

Kama kuna mtu kakwambia, Flani njoo kesho nikulipe deni lako Basi wewe usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na ww umeahidiwa

3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia.

Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki.

4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa. Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo.

Maarifa ndio mtaji wa kwanza. Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema, "Omba ndoano, usiombe samaki"

5. Usitunze mbegu badala ya kuipanda. Watu wengi hufurahia pesa wanayolipwa/kuipata kisha wanaiweka bank au nyumbani bila kuiwekeza. Wekeza pesa ili uzalishe zaidi. Usiogope kuingia hasara, kila aliyefanikiwa alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa. Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa”

6. Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo unahisi hatorudisha.
Unapomkopesha mtu huyo pesa, jiridhishe mwenyewe moyoni kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake-halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri aende bank akakope”

7. Usikubali kumdamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile unachomdhamini.
Kumbuka- dhamana maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa.

8. Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo.
Unaweza kujikuta unafanya matumizi ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni.
Ili kuepuka haya, tembea na pesa uliyopanga kuitumia katika safari yako. Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo salama”

9. Epuka kutunza pesa mahali pasipo sahihi.
Maeneo kama kwenye soksi, sidiria, chini ya mto wa kulalia, chini ya begi, kwenye kopo au hata kwenye begi la safari, si maeneo salama. Ni rahisi kusahau, kuibiwa au kupoteza pesa zako.

Ni bora ukatunza pesa kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo kwenye nguo zako hasa uwapo safarini.

10. Usitumie pesa kwa kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba yako.
iulize kwanza kabla hujanunua,
"Bila kitu hiki, maisha yataenda au lah?”
Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.

11. Matumizi yako ya pesa yasizidi pato lako.

Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato lako.

Unapaswa kuwa bahili katika matumizi yako. Cheza na pato lako.
Fanya matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka. Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa.

12. Una ndoto kubwa hapo baadae; labda kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki.

Usikurupuke, ukanunua kitu cha ndoto yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo.

Usichanganye kati ya mahitaji ya baadae na ya sasa.

Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto. Hii itakuepushia kuingia katika madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa.
Jipange taratibu kutimiza ndoto yako.

Comments

Popular posts from this blog

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

UGONJWA WA ZINAA WA KISONONO(GONORRHEA) DALILI ZAKE, MADHARA YAKE NA JINSI YA KUJIKINGQ

Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi sana duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono.  Vitendo hivi vya ngono vinaweza kuwa kujamiana, kupiga denda (kissing), vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral genital sex), kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe kwa mwanamume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators).  Magonjwa ya zinaa huathiri sana watu walio katika umri wa miaka 15 – 24 lakini hata kwa watu wengine ambao wana umri chini au zaidi ya huu niliotaja pia yanaonekana kwa wingi. Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya ishirini yanayotambulika duniani, baadhi ya magonjwa ya zinaa ni  Kisonono (Gonorrhoea – “Gono” kama wengi wanavyopenda kuita kwa kifupi).     Chlamydia     Kaswende (Syphillis)     Human papilloma virus (HPV)     HIV/AIDS (Ukimwi/Upungufu wa kinga mwilini)     Hepatitis B, C, A     Herpes vi

HII INAITWA FUNGA MWAKA NA PARTY LA KIJANJA LA NIT FRESHES PARTY LIVE NDANI YA JANGWANI SEA BREEZY LIMEANDALIWA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI SONIT

Huyu ndiye atakaye kuwa host wetu katika party la kijanja la NIT fresher's party linano waunganisha wanafunzi wote wa NIT Pia kutakuwa na michezo mbali mbali itakuwa ikiendelea ndani ya jangwani sea breeze