Skip to main content

Posts

MBINU ZA KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA

Kwanza kabisa ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara ambayo unaifanya unatakiwa kuachana na mfumo wa zamani ambao ulikuwa unatumia katika kufanya biashara yako, kama inashindikana kuachana na mfumo huo wa zamani basi unachotakiwa kufanya ni kuboresha mfumo huo wa zamani ili uweze kufanikiwa kibiashara. Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa kulikumbatia katika biashara yako ni,  kuelewa mbinu za kufanya biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii.  Kwa wenzetu wazungu mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia kutengeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani. Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi dunia ya s...

ZIJUE TABIA ZA WATU WENYE WIVU

Mara mtu apatapo mafanikio mambo mengi hutokea au hubadilika. Moja kati ya mambo ambayo hutokea ni mabadiliko kwa watu wanao mzunguka mtu huyo. Wengine humpenda, wengine humheshimu, wengine humchukia au hata kumwonea wivu. Wivu umekuwa ukitesa na kurudisha maendeleo ya watu nyuma hasa wale ambao ndio huwa na wivu huo mioyoni mwao. Kwa kuwa wivu hauwaathiri wale walio nao pekee, ni vyema nawe ukafahamu tabia za watu wenye wivu ili uwaepuke wasije wakakuathiri kwa kukurudisha nyuma katika hatua zako za maendeleo. 1. Hawastaajabishwi na mafanikio ya wengine Moja kati ya tabia kubwa ya watu wenye wivu ni kutostaajabishwa na mafanikio ya wengine. Wao hata wasikie jambo zuri au kubwa kiasi gani la mtu mwingine wao hujifanya kuliona kama la kawaida tu. Unaweza kusikia hata wakisema kauli kama vile “mbona hayo mambo ya kawaida”, “mbona wapo wengi waliofikia hapo”, “mambo ya kupita hayo, cha muhimu uzima bwana”, “mafanikio ya watu hayanihusu bwana”, n.k. Watu wenye tabia kama hii ni wakuep...

FAIDA ZITOKANAZO NA ULAJI WA PARACHICHI KIAFYA

Parachichi ni tunda lisilo na ladha ya sukari linalopendwa na watu wengi. Watumiaji wanalitumia kwa namna tofauti. Wapo wanaokula baada ya kulimenya, wengine hulitengenezea juisi huku wengine wakilitumia kula kama mboga kwa kulichanganya kwenye vyakula hususan wali. Tunda hilo lenye virutubisho vingi na muhimu kwa afya ya binadamu, linaelezwa na wataalam wa afya kuwa lina msaada mkubwa katika kulinda afya ya binadamu. Parachichi linaelezwa kuwa ni mbadala wa vyakula vya nyama kwa jinsi lilivyo na malighafi zote zilizo muhimu ndani yake. Tunda hilo linapotengenezwa kama kinywaji (juisi) husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha udhaifu mwingine tumboni. Tunda hili linapotumiwa linasaidia kuongeza nguvu za mwili na ubongo sanjari na kujenga neva za fahamu. Pia linampa mtu uwezo wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza damu. Si hivyo tu, majani hayo yamesheheni wingi wa vitamini A, B, C na E. Mandai anasema vyakula kama nyama vinasa...

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO 18/11/2019

MWANZILISHI WA ALIBABA AWAASA WAJASIRIAMALI VIJANA WA AFRIKA

Mwanzilishi wa kampuni ya biashara ya mtandaoni ya China Alibaba, Jack Ma amesema mfuko wake utaendelea kuwaunga mkono wajasiriamali vijana wa Afrika. Jack Ma amesema hayo baada ya kutoa tuzo zenye thamani ya dola milioni moja kwa wajasiriamali 10 vijana wa Afrika kwenye tuzo za kwanza za wajasiriamali kupitia mtandao wa internet, zilizotolewa Jumamosi mjini Accra, Ghana. Akiongea kwenye hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Jack Ma amesema kama Afrika ikitaka kuwa na ongezeko endelevu, jambo muhimu ni kwa wajasiriamali hao kuwa na njia za uvumbuzi. Rais Akufo-Addo wa Ghana amesema kwenye hafla hiyo kuwa ujasiriamali unatakiwa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa ili kuhimiza utamaduni wa ujasiriliamali.

MIPANGO YA KUIFAHAMU KABLA YA KUANZISHA BIASHARA

MipaMalengo ni lazima yaende sambamba na mipango ili kuweza kutimiza ndoto zako kibiashara, hata hivyo huenda ukawa haujanielewa, ipo hivi, mipango ni mtiriko wa namna ya kuyafikia malengo. Pia malengo ni lazima yaanze katika ngazi ya chini kabisa, hapa nikiwa na maana ni lazima uanze na malengo madogo madogo au watalaamu wa masuala ya mafanikio huita (baby step). Malengo ya kibiashara ni njia sahihi ya kufanikiwa kwako kibiashara, kuna baadhi ya watu wao hufanya mambo ambayo hayana mipango na mikakati ambayo itawasababisha kuweza kutimiza ndoto zao ambazo wamejipangia katika masuala mazima ya kibiashara. Na kufanya hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, kwani kila siku utajiona ni mnyonge, huna faida za kuendelea kuishi, hufai hii ni kutoka na kutoiona faida yeyote katika biashara ambayo unaifanya. Yafutayo ni maswali muhimu ambayo ni muhimu kujiuliza  katika upangaji wa malengo ya uanzishaji kibiashara; 1. Eneo kwa ajili ya kufanyia biashara. Kuanzisha biashara mpya ni ...

HUYU NDIYE MWANAMKE ANAYELIPWA MSHAHARA MKUBWA ZAIDI DUNIANI

Denise Coates hulipwa mshahara wa zaidi ya Pauni za Uingereza 265 milioni (zaidi ya Shilling 340 bilioni).mwanamama huyu Ni Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya kamari ya Bet 365 Aidha, Coates ni kati ya watu matajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola 4.1 bilioni.Kitita cha mshahara anaolipwa Coates zikiwa zimepangwa katika noti za 1000 zinaweza kufanya mnara mrefu zaidi ya jumba la Times Times Tower. Mshahara wa Coates ni zaidi ya mara tatu anachopata mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook ambaye alipokea £ 80 (zaidi ya bilioni 10.5).Tofauti hii inatiliwa maanani ikizingatiwa Apple ndiyo kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani. Kulingana na mtandao wa Guardian, mapato ya Bet 365 yalifika 52 billioni ( zaidi ya 6.8 trilioni), pato ambalo limepita pato jumla la mataifa kama Uruguay, Croatia na hata Kenya. Aidha, kuchora taswira kamili mshahara wa Bi Coates wa miaka 10 unaweza kulipia deni la reli ya kisasa ya SGR kutoka dar kwenda dom Aidha kampuni ya Bet365 ndiyo ambayo ...

NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO

Job Opportunity at Epic Business Resources Limited, Maintenance Manager Volunteering Opportunities at Active Women Foundation (AWF) Job Opportunity at Aga Khan,Clinical Epidemiologist Job Opportunity at Alistair Group, Driver Trainer Tanzania Job Opportunity at Center for Strategic Litigation’s (CSL), Finance Administrative Assistant 5 Job Opportunities at CRDB - Contact Centre Agent

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO 17/11/2019

FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA POLIO KIUNDANI ZAIDI

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza usababishwao na virusi, huathiri neva na kusababisha ulemavu. Kutokana na taarifa za shirika la afya duniani: Polio huathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano Ulemavu hutokea kwa mmoja kati ya maambukizi 200 Mpaka 2013 ni nchi tatu ambazo bado kuna mlipuko wa ugonjwa huu wa kupooza Afghanistan, Pakistan na Nigeria. Ila kutokana na Taarifa kutoka wizara ya afya ya Tanzania ilipokea taarifa kutoka shirika la afya duniani kuwa kuna mlipuko katika nji jirani ya Kenya, wilaya ya Fafi. Je ni zipi dalili za ugonjwa huu? Dalili hizi hudumu kwa kati ya siku 1 hadi 10 Homa Maumivu ya kichwa Kutapika Uchovu Maumivu ya shingo Maumivu ya mgongo Maumivu ya mikono na miguu Misuli kukakamaa Je ni matatizo gani mtu huweza kupata baada ya maambukizi haya? Kupooza misuli Ulemavu wa miguu Vipimo: Virusi vya polio huweza kuonekana katika makohozi, kinyesi na maji maji ya uti wa mgongo. Matibabu Hamna matibabu ya maambukizi haya, kwahiyo ni tiba ya dalili amba...

WIZARA YA KILIMO WAKUTANA NA WADAU WA KILIMO CHA TUMBAKU NCHINI

Wizara ya Kilimo imekutana na wadau na wakulima wa kilimo cha Tumbaku hapa nchini ili kujadili changamoto zilizopo katika sekta hiyo nakuzitatua ili kuinua sekta ya kilimo cha Tumbaku hapa nchi. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma na kuwakutanisha Wizara ya kilimo, fedha na wadau wa kilimo cha Tumbaku, wakulima na makampuni yanayonunua zao la Tumbaku na wenye viwanda vya Tumbaku, naibu Waziri wa Kilimo Husain Bashe. Amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha Wanakutana kwa pamoja na kujadili changamoto na vikwazo vyote vinavyopelekea kutoendelea kwa kilimo cha Tumbaku hapa nchi pamoja na ili kwa pamoja kuona namna ya kuondoka hapa tulipo. "Tumekutana hapa lengo likiwa ni kuangalia ni namna gani tunaweza kutoka hapa tulipo na kwenda mbele, ndio maana tumeshirikisha wadau wote sisi Wizara ya kilimo, fedha, wadau wa kilimo,wenye viwanda na wakulima ili kila mtu ajue nani ni kikwazo na kuanguka kwa sekta hii" Ameongeza...

JINSI YA KUFANIKIWA KIMAISHA KUPITIA KILIMO CHA NYANYA

Habari ndugu msomaji wa wetu wa makala za kilimo, Natumaini tunaendelea vizuri na mapambano ya kila siku. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote: Utangulizi Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu. Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda,Tanzania, Rwanda na Burundi Zao la nyanya linali...