Skip to main content

FAIDA ZITOKANAZO NA ULAJI WA PARACHICHI KIAFYA


Parachichi ni tunda lisilo na ladha ya sukari linalopendwa na watu wengi. Watumiaji wanalitumia kwa namna tofauti.

Wapo wanaokula baada ya kulimenya, wengine hulitengenezea juisi huku wengine wakilitumia kula kama mboga kwa kulichanganya kwenye vyakula hususan wali.

Tunda hilo lenye virutubisho vingi na muhimu kwa afya ya binadamu, linaelezwa na wataalam wa afya kuwa lina msaada mkubwa katika kulinda afya ya binadamu.

Parachichi linaelezwa kuwa ni mbadala wa vyakula vya nyama kwa jinsi lilivyo na malighafi zote zilizo muhimu ndani yake.

Tunda hilo linapotengenezwa kama kinywaji (juisi) husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha udhaifu mwingine tumboni.

Tunda hili linapotumiwa linasaidia kuongeza nguvu za mwili na ubongo sanjari na kujenga neva za fahamu. Pia linampa mtu uwezo wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza damu.

Si hivyo tu, majani hayo yamesheheni wingi wa vitamini A, B, C na E. Mandai anasema vyakula kama nyama vinasababisha 'asidi ya yuriki ' nyingi mwilini ambayo ni chanzo cha magonjwa mengi.

Tunda hilo likitumiwa kwa maelekezo ya kitaalamu linaweza kusafisha na kuitoa asidi hiyo na hivyo kumwacha mlaji katika uhakika wa kuondokana na tishio la magonjwa ambayo yangeweza kumpata.

Tunda hili hufanya vizuri kwa magonjwa hayo na kuyamaliza, lakini pia linasaidia wanawake  kuifanya hedhi iende vizuri kila mwezi,.

Pia majani ya parachichi yanapochemshwa na kunywewa kama chai yanasaidia kuondoa matatizo mwilini, ikiwa ni pamoja na uchovu, udhaifu na kujisikia ovyo, kuumwa kichwa, koo, tumbo, mapafu na uvimbe.

Hali kadhalika, unapotafuna majani yake husaidia kutibu vidonda vya mdomo (ufizi) na kuimarisha meno pamoja na kuondoa maumivu.

Pamoja na hayo, parachichi pia linaweza kutumika hata katika masuala ya urembo, linasaidia mwenye tatizo la nywele kukatika.

Mtaalam huyo anasema hizo ni baadhi tu ya faida nyingi za parachichi tunda linastawishwa kwa wingi zaidi katika mikoa kadhaa hapa nchini ukiwemo Kilimanjaro na Tanga.

Anatoa mwito kwa jamii kupenda kutumia matunda kutokana na umuhimu wake katika kulinda afya zao.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.