Skip to main content

MBINU ZA KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA


Kwanza kabisa ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara ambayo unaifanya unatakiwa kuachana na mfumo wa zamani ambao ulikuwa unatumia katika kufanya biashara yako, kama inashindikana kuachana na mfumo huo wa zamani basi unachotakiwa kufanya ni kuboresha mfumo huo wa zamani ili uweze kufanikiwa kibiashara.

Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa kulikumbatia katika biashara yako ni,  kuelewa mbinu za kufanya biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii.  Kwa wenzetu wazungu mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia kutengeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani.

Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi dunia ya sasa inakwenda kasi sana tofauti na ilivyokuwa nyuma.

Na ili uweze kwenda sawa na kasi hiyo ni lazima jifunze mbinu mbalimbali zitakazokusaidia kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwani kwa sasa wanaitumia njia hiyo ndiyo ambao wanafaidi matunda ya kutumia mbinu hizo.

Jambo jingine ambalo litaweza kukusaidia kuweza kuongeza mauzo ya katika biashara unayoifanya ni kuhakikisha unakuwa mtalamu katika biashara husika. Hii mbinu muhimu sana katika kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara kwa sababu pindi utakapokuwa mtalamu au m-bobezi wa jambo hilo itakusaidia sana kuweza kuizungumzia vizuri bidhaa au huduma unayoitoa kwa mteja wako,  kufanya hivyo kutamfanya mteja huyo ainunue bidhaa hiyo. Hivyo ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara yako jifunze kuwa mtalamu katika eneo husika unalolifanya.

Jambo la mwisho ambalo ni muhimu sana litakalo kusaidia kuweza kufanya biashara yenye tija ni kuhakikisha unaimarisha vizuri upande wa huduma kwa mteja, kwa sababu ule usemi wa kwamba mfalme ni mteja hakuwepo tu, bali msemo huo upo kumanisha kweli, mteja ni mfalme pindi awapo na asipokuwapo katika eneo lako la kibiashara pia.

Ufike pahala neno  mteja liwe lina maana kubwa sana katika biashara yako, yaani mfanye mteja kuwa ni sehemu ya biashara ya yako. Mfanye mteja ajisikie huru katika suala zima la kibiashara.

Mwisho nimalize kwa kusema biashara yenye tija hujengwa na vitu vitatu vya msingi ambavyo ni bidhaa au huduma nzuri+ masoko mazuri= wateja wengi.

Na. Benson Chonya


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.

NAFASI 37 ZA KAZI TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) DEADLINE 29/11/2019

The Tanzania Institute of Accountancy (TIA) is an Executive Agency under the Ministry of Finance and Planning which was established on 1st July, 2002 by the Government Notice No. 489 of 1st November, 2001 and officially launched on 24th January, 2002 as per Act No. 30 of 1997. As an Executive Agency, TIA is operating ‘semi’ autonomously and commercially in providing quality education in the field of Accountancy, Procurement & Supplies and other Business related disciplines so as to become a self-sustainable Institute. TIA is accredited by NACTE as an Institute of Higher Learning Education. ==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi ; << Ingia Ha>> The Institute is looking for qualified and dedicated personnel to fill the post of Tutorial Assistants on contract basis. The table below provides details on a particular fields/ professionals one should apply against. ==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi ; << Ingia Ha>>