Skip to main content

Posts

BEI NDOGO YAKATISHA TAMAA WAKULIMA WA KAHAWA.

Wakulima wa zao la kahawa wa kata ya Mugoma wilayani Ngara mkoani Kagera wamekatishwa tamaa na zao Hilo kutokana na kushuka bei kwakiasi kikubwa. Wakizungumza na Muungwana Blog baadhi ya wakulima hao wamesema kuwa zao hilo limeshuka bei wakati wa uuzaji wao kwani mwaka jana kahawa Kg1 ilikuwa ikiuzwa 1800 lakini kwasasa huuzwa Kg1 1100. Wamesema hali hiyo ya uuzaji wa kahawa inawakatisha tamaa kama wakulima kwani kahawa ndio tegemezi lao katika maisha yao ya kila siku. Gedion ambaye ni mkulima wa zao hilo amesema kuwa kahawa imeshuka kiasi kikubwa hali ambayo inapelekea kutokujikwamua kiuchumi. Shukuru ambaye pia ni mkulima  amesema zao hilo limemewakatisha tamaa kutokana nakushuka bei mara kwa Mara wakati wa uuzaji wao kwa wafanyabiashara. "Kama mwaka huu zao kahawa Kg1 1100 na mwaka jana ilikuwa Kg1 1800 unaona ni jinsi gani tunapata hasara wakati wa uuzaji wetu wakati tunatumia gharama kubwa wakati wakulima." Amesema Shukuru Cosmas Bishundu ni mwenyekiti wa kitongoji c...

UZALISHAJI WA MAKAA YA MAWE WAONGEZEKA NCHINI

Imeelezwa kuwa, wastani wa uzalishaji wa Makaa wa Mawe nchini umekuwa ukiongezeka tofauti na ilivyokuwa  awali huku sababu kadhaa zikichangia ongezeko la uzalishaji huo ikiwemo mazingira mazuri ya uwekezaji, zuio la  Serikali kuingiza makaa ya mawe kutoka nje, ongezeko la viwanda vinavyotumia makaa ya mawe na  kuboreshwa kwa mundombinu ya usafirishaji.    Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa wakati akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu  hatua zilizofikiwa katika  uendelezaji wa miradi ya makaa ya mawe kwa niaba ya Waziri wa Madini.   Mhandisi Mulabwa amesema katika kipindi cha miaka 8 kuanzia mwaka 2011 hadi 2018, uzalishaji uliongezeka kutoka tani 81,384.67 mwaka 2011 na kufikia  627, 651.00 mwaka 2018, ikiwa ni  wastani wa takribani tani 52,304.25 kwa mwezi.   ‘’ Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miezi 9 kwa mwaka 2019, uzalishaji  uliongezek...

VICHWA VYA MAGAZETINI LEO 28/10/2019

FAHAMU NJIA 16 ZA KUONDOA SUMU MBALIMBALI MWILINI

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali. Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako. Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini 1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee Amua moja ya mlo wako kwa siku uwe ni matunda pekee bila chakula kingine zaidi. Unaweza kuamua ama chakula cha asubuhi au cha jioni kuwa ni matunda pekee, ndiyo kwenye sahani yako unajaza matunda tu mbalimbali sahani ijae na ule hayo tu kama ndiyo mlo wako ukimaliza unaweza kunywa juisi ya matunda au maji pekee. 2. Kula vyakula vya asili zaidi kuliko vya viwandani Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia kati...

TBS YATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetumia Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani kwa kutoa elimu, kusikiliza changamoto za wenye viwanda, wazalishaji na wajasiriamali na kuzipatia ufumbuzi ili kuhakikisha wanaendelea kufanya uzalishaji kwa kufuata mifumo sahihi. Maofisa hao walikutana na wadau hao katika ofisi za SIDO, Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo pia waliwahamasisha kushiriki katika uandaaji viwango. Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) ambalo TBS ni mwanachama, huadhimisha Siku ya Viwango Duniani kila mwaka Oktoba 14, lakini kwa Tanzania kutokana na siku hiyo kuangukia tarehe ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, TBS ilisogeza mbele maadhimisho hayo hadi kuanzia Oktoba 21 na yanatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 31, mwaka huu. Ofisa Viwango Mwandamizi wa TBS, Joseph Mwaipaja, alisema wanatumia fursa hiyo kumbusha wadau umuhimu wa viwango, lengo likiwa ni kupunguza bidhaa zisizofaa katika masoko ya Tanzania na kuwajengea wananchi, wenye viw...

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUFANYA BIASHARA YENYA MAFANIKIO

Kila mfanyabiashara anatamani kuona anafanya biashara ambayo ina mafanikio, hivyo ili kufanya biashara ya yenye mafanikio, yafutayo ndiyo mambo ya muhimu ya kuzingatia katika kufanya biashara yenye mafanikio: 1. Fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuazisha siyo tu kwa kuwa kuna mtu unayemjua amefanikiwa kutokana na biashara hiyo. Pia hakikisha unajua ni nini utakifanya endapo biashara hiyo itaanguka ghafla. 2. Uwe tayari kufanya maamuzi magumu! Daima kuwa mtu wa kuthubutu na usiogope hasara kwani mafanikio huanza kwa taratibu na hasara ni njia moja wapo ya kujifunza na kuendelea mbele katika biashara. 3. Mafanikio huanza kwa kiasi kidogo cha fedha, usiache kuthubutu kwa kuwa tu, hauna mamilioni ya pesa ya kuanzia kama mtaji. Siku zote hakikisha una fedha za dharula na kamwe usitumie fedha ya mtaji kwa matumizi mengine. 4. Jitahidi kadri ya uwezo wako kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ambayo yatapelea kuharibu mtaji wako ulioanza nao. 5. Unapokuwa unafanya mpango mk...

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO 27/10/2019

NAFASI MBALIMBALI ZA KAZI KUTANGAZWA LEO TANROADS CHUO KIKUU SAUTI, MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TCAA

==>>Nafasi Mpya za kazi  Zilizotangazwa na TANROADS - Mtwara. 👉Wanahitajika Watu wa fani Mbalimbali. 👉Elimu ni kuanzia kidato cha Nne 👉Deadline; 01 November 2019. Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ ==>>Nafasi Mpya za  kazi Zilizotangazwa na Chuo Kikuu cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) - Mwanza. 👉Wanahitajika Watu wa Fani Mbalimbali 👉Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe; 01 November 2019. Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ ==>>Nafasi 16  Za Kazi toka Mamlaka Ya Usafiri Wa Anga -TCAA 👉Wanahitajika Watu wa Fani Mbalimbali 👉Elimu: kuanzia ya Cerificate /Diploma 👉Deadline: November 06,2019 Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ l

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO 26/10/2019