Skip to main content

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUFANYA BIASHARA YENYA MAFANIKIO



Kila mfanyabiashara anatamani kuona anafanya biashara ambayo ina mafanikio, hivyo ili kufanya biashara ya yenye mafanikio, yafutayo ndiyo mambo ya muhimu ya kuzingatia katika kufanya biashara yenye mafanikio:

1. Fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuazisha siyo tu kwa kuwa kuna mtu unayemjua amefanikiwa kutokana na biashara hiyo. Pia hakikisha unajua ni nini utakifanya endapo biashara hiyo itaanguka ghafla.

2. Uwe tayari kufanya maamuzi magumu! Daima kuwa mtu wa kuthubutu na usiogope hasara kwani mafanikio huanza kwa taratibu na hasara ni njia moja wapo ya kujifunza na kuendelea mbele katika biashara.

3. Mafanikio huanza kwa kiasi kidogo cha fedha, usiache kuthubutu kwa kuwa tu, hauna mamilioni ya pesa ya kuanzia kama mtaji. Siku zote hakikisha una fedha za dharula na kamwe usitumie fedha ya mtaji kwa matumizi mengine.

4. Jitahidi kadri ya uwezo wako kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ambayo yatapelea kuharibu mtaji wako ulioanza nao.

5. Unapokuwa unafanya mpango mkakati wa fedha jitahidi matumizi yako uyawekee makadirio ya juu na kipato chako ukiwekee makadirio ya chini.

6. Kama unataka kufanya biashara na huduma ambayo kuna wengine wanafanya, hakikisha biashara yako iwe na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na watu wengine, na ujue wanakosea wapi na utafanya nini cha tofauti la sivyo utakuwa nyuma yao milele kwani kinachowavuta watu kuja kununa kwako ni utofauti kati yako na wapinzani wako na sio tu kwa kuwa bidhaa unayo.

7. Fanya utafiti sokoni kujua watu wanazichulia vipi bidhaa au huduma unayotaka kutoa ili kuweza kujua wapi unakosea na kujirekebisha mapema iwezekanavyo ili kuendelea kutengeneza mahusiano mazuri na watu.

8. Hakikisha jina la biashara yako linamvuto na kukubalika katika jamii husika. Pia Jihusishe na watu mbalimbali walioendelea katika ujasiliamali ili uweze kupata mawazo mbalimbali na mbinu mpya za kuweza kufanikiwa katika ujasiliamali.

9. Andika! Mali bila daftari huisha bila habari. Daima tunza kumbukumbu zako katika maandishi

10.Tafuta kitu kitakachokuwa na ushawishi wa hali ya juu kwa wakati huo katika eneo husika, ukitumie kama njia ya kujitangaza. ukifanikiwa katika hilo basi utajijengea channel kubwa na watu wengi watakujua na hiyo itakurahisishia safari ya kufahamika

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.

NAFASI 37 ZA KAZI TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) DEADLINE 29/11/2019

The Tanzania Institute of Accountancy (TIA) is an Executive Agency under the Ministry of Finance and Planning which was established on 1st July, 2002 by the Government Notice No. 489 of 1st November, 2001 and officially launched on 24th January, 2002 as per Act No. 30 of 1997. As an Executive Agency, TIA is operating ‘semi’ autonomously and commercially in providing quality education in the field of Accountancy, Procurement & Supplies and other Business related disciplines so as to become a self-sustainable Institute. TIA is accredited by NACTE as an Institute of Higher Learning Education. ==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi ; << Ingia Ha>> The Institute is looking for qualified and dedicated personnel to fill the post of Tutorial Assistants on contract basis. The table below provides details on a particular fields/ professionals one should apply against. ==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi ; << Ingia Ha>>