Skip to main content

BEI NDOGO YAKATISHA TAMAA WAKULIMA WA KAHAWA.


Wakulima wa zao la kahawa wa kata ya Mugoma wilayani Ngara mkoani Kagera wamekatishwa tamaa na zao Hilo kutokana na kushuka bei kwakiasi kikubwa.

Wakizungumza na Muungwana Blog baadhi ya wakulima hao wamesema kuwa zao hilo limeshuka bei wakati wa uuzaji wao kwani mwaka jana kahawa Kg1 ilikuwa ikiuzwa 1800 lakini kwasasa huuzwa Kg1 1100.

Wamesema hali hiyo ya uuzaji wa kahawa inawakatisha tamaa kama wakulima kwani kahawa ndio tegemezi lao katika maisha yao ya kila siku.

Gedion ambaye ni mkulima wa zao hilo amesema kuwa kahawa imeshuka kiasi kikubwa hali ambayo inapelekea kutokujikwamua kiuchumi.

Shukuru ambaye pia ni mkulima  amesema zao hilo limemewakatisha tamaa kutokana nakushuka bei mara kwa Mara wakati wa uuzaji wao kwa wafanyabiashara.

"Kama mwaka huu zao kahawa Kg1 1100 na mwaka jana ilikuwa Kg1 1800 unaona ni jinsi gani tunapata hasara wakati wa uuzaji wetu wakati tunatumia gharama kubwa wakati wakulima." Amesema Shukuru

Cosmas Bishundu ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mkagugo kijiji cha Mruvyagira kata ya Mugoma amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa wakulima hao nakuwatoa wasiwasi kwani tatizo hilo ashalifikisha kwa viongozi wa juu nalinafanyiwa kazi.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.