Miasha ya mwanadamu yamejawa na changamoto na shida mbalimbali. Changamoto hizo hizo, wapo baadhi ya watu huzivumilia katika kutenda jambo fulani, lakini pia wapo baadhi ya watu hukta tamaa kabisa. Na hao ambao hukata tamaa ndio ile idadi kubwa ya watu ambao hufa na ndoto zao mapema.
Lakini ukweli ni kwamba changamoto na shinda mbalimbali za maisha ni kipimo cha akili, kwani wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo huimba katika nyimbo zao na kusema changamoto ni majaribu, na majribu ni mtaji. Hivyo katika maisha haya ni jambo la ajabu sana kama utaendelea kukataa tamaa kwa sababu ya changamoto Fulani.
Na ukweli ni kwamba ili uweze kufanikiwa wanasema changamoto hazikwepeki, na changamoto ndio njia ambayo itakufikisha kule ambapo unataka kufika, endapo tu utaamua kupambana na changamoto hizo.
Swali linakuja nawezaje kupambana na changamoto hizo?
Jambo la msingi unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapambana na changamoto za maisha ni;
1. Orodhesha changamoto zote ambazo zinakukubali. Hata kama zipo zaidi ya changamoto tano ainisha zote.
2. Baada ya kuorodhesha changamoto hizo tano, jambo ambalo unatakiwa kufanya baada ya hapo unatakiwa kuchugua jambo ambalo lina umuhimu sana katika kulitekeleza.
3. Baada ya kulipata jambo hilo, usiishie kulichagua tu. Tafuta mbinu ya jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo. Na mbinu hizo ziandikwe mahali ambapo panaonekana na uanze utekelezaji mara moja.
Mbinu hii ya kupambana na changamoto itakusaidia sana katika kupiga hatua mbele zaidi kivitendo kuliko kukata tamaa.
Nimekupa mbinu hii, kwa sababu wengi wengi huwa tunajitenga na chanagamoto za kimaisha hasa pale zinapojitokeza. Lakini kama nilivyoeleza hapo awali ni kwamba changamoto za kimaisha ni kigezo tosha cha kuweza kutimiza ndoto yako, jambo la msingi tafuta majibu ya jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo.
Kama hutatafuta majibu ya changamoto zinazokukabli itakuwa ni sawa na bure, kwani utazidi kuwa maskini maisha yako yote.
Comments
Post a Comment
Yes