Skip to main content

FAHAMU KANUNI ZA MAISHA BORA



Kila kitu kina misingi na kanuni zake, maisha nayo yana misingi na kanuni zake. Ili uweze kuishi na kufurahia maisha katika kiwango cha juu unatakiwa kufahamu na kuishi misingi na kanuni.

Hizi ni ambazo nimezifanya ziwe kama mwongozo wako;


  1. Afya : Afya ya Mwili. Afya ya Akili. Afya ya Kiroho. Vitu Hivi vitatu ni muhimu sana kwenye maisha yako. Huwezi kusema una maisha bora kama hizi sehemu tatu hazina ubora au hazina afya.Unapaswa kuwa na mikakati ya kufanyia kazi sehemu hizi kwasababu ndio zimebeba maisha yako yote
  2. Hekima :Wakati Sahihi wa Kukaa Kimya. Wakati Sahihi wa Kuongea Kitu Sahihi Cha Kuongea. Hii itakuwezesha uweze kuishi na wengine vizuri. Kuna watu wenye tabia mbalimbali zinazokera bila ya Hekima utakuwa mtu mwenye hasira, chuki na Visasi hutaweza kufurahia maisha.
  3. Utajiri : Uwekezaji, Mali, Mtandao wa Watu, Upendo.Maisha ili yawe bora ni lazima ufikie kile kiwango ambacho Hutakuwa na Matatizo yanayoletwa na ukosefu wa pesa.Hivyo ni muhimu kuhakikisha vile ambavyo unatakiwa kuvifanyia kazi ili kujenga mifereji ya kipato ambayo inadumu.


Huwezi kuvipata hivyo pasipo na maarifa Sahihi, kuwa na malengo, kuchukua hatua kubwa, kutokuishia njiani.

Yakupasa uwe mvumilivu, usiwe mtu wa kuyumbishwa na yale yanayotokea bali uwe mtu unaesimamia misingi ya kile unachokiamini.Karibu Sana Rafiki katika safari ya kutengeneza Maisha bora

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.