Bila kuku kulishwa chakula bora na kupewa maji safi , salama,yasiyokuwa moto na yanayopatikana muda wote wa mchana na usiku , usitegemee mayai mengi wala nyama nyingi ,laini na nyeupe.
Ulishaji bora uanzie kwa vifaranga wa siku moja hadi kipindi chote cha utagaji au kuku kuuzwa kwaajiri ya kuchinjwa.
Chakula bora cha kuku ni mchanganyiko maalum uliozingatia uwiano wa:-
Vyakula vya aina ya protin (protin nyama, protin mimea) kwa kujenga mwili na kuunda sehemu za mwili zilizoharibika.
Madini kama chumvi na chokaa kwa kujenga mifupa na kutengeneza makaka ya mayai.
Vyakula vya wanga kwa kutia nguvu mwili wa kuku.
Mchanga kwaajili ya kusaga chakula
Vitamin kwa kutia afya mwili na kumfanya kuku awe mchangamfu
Kazi ya maji ni kuwezesha chakula hicho kumeng'enywa ili kiweze kuingia mwilini na kufanya kazi iliyokusudiwa.
Faida za chakula bora .
Kuku hukua haraka
Kuku hukomaa mapema
Kuku huwa na afya nzuri
Kuku kutaga mayai mengi,makubwa na yenye makaka magumu
Utagaji huendelea kwa muda mrefu
Nyama huwa nyingi,laini na nyeupe
Uzito wa kuku huongezeka
Comments
Post a Comment
Yes