Skip to main content

SERIKALI YALETA MFUMO MPYA KUKUSANYA TAARIFA ZA KIBIASHARA


Eric Msuya – MAELEZO
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Stellah Manyanya amewataka wadau wa Sekta hiyo kutumia mfumo mpya wa kukusanya Taarirfa za Kibiashara Nchini kwa lengo la kupiga hatua kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati. 
 
Kuanzishwa kwa mfumo huo ujulikanao kama Trade Information Module, ni utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa yaliyopo kwenye mkataba wa uwezashaji wa Kibiashara unaosimamiwa na Shirika la Biashara Duniani. 
 
Manyanya aliyasema hayo jana, Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Wafanyabaishara na Wadau wa Biashara,  kuhusu mfumo wa utoaji wa Taarifa za Kibiashara Nchini, ambapo alisema, mfumo huo mpya utasaidia utunzanzaji na upatikanaji  wa taarifa za Leseni pamoja na Vibali mbalimbali vya kufanyia Biashara Nchini. 
 
“Kama manavyojua, upatikanaji wa Taarifa ni muhimu sana katika kufanya maaamuzi ya kila jambo hivyo  uwepo wa Taarifa hizi za Biashara mahali pamoja utasaidia Wafanyabiashara kujua mahitaji, utaratibu na mahali pa kupata vibali mbalimbali” alisema  Mhe. Stellah 
 
Alisema mfumo huu utaliwezesha Taifa kupata Fedha za kigeni sambamba na kumsaidia mfanyabiashara kujua taratibu na masharti ya kuingiza Bidhaa zao Nchini kupitia Masoko ya Nje ya Nchi. 
 
Sambamba na hilo, Mhe. Stellah aliwataka Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali kutumia mfumo huo vizuri kwani utaleta Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Biashara Nchini pamoja na kuondoa kero mbalimbali. 
 
“Lakini pia mfumo huu utaongeza ukaribu baina ya Wafanyabaishara na Ofisi za Umma, utaongeza ufanisi na kupunguza gharama za Kibiashara, utapunguza muda anaotumia Mfanyabiashara kupata Leseni,  hivyo kwa ujumla mfumo huu utaboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini kwa kuchangia Uchumi wa Nchi” alisema Mhe Stellah. 
 
Pamoja na hilo, Serikali ya awamu ya Tano, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za za kuboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini (Blueprint  For Regulatory Reform to Improve Business Environment)  ili kuweza kuwavutia  wawekezaji wa ndani na Nje ya Nchi kuja kuwekeza  hapa kiurahisi. 
 
“tunafanya jitihada nyingi sana ili kuboresha mazingira nchini hususan mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania” alisema Manyanya. 
 
MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.