Skip to main content

JINSI YA KUANDIKA CV NZURI AMBAYO ITAMVUTIA MWAJIRI NA KUKUFANYA UPATE KAZI


WATU Wengi nchini wamekosa ajira na makampuni hupokea wastani wa maombi 200 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Hivyo, CV yako lazima ikae vizuri ili kumshawishi mwajiri. Utaratibu wa kuomba kazi inaweza ikawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.

CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.

Mambo yafuatayo yatasaidia kuifanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview za kazi.

👉Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.

Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.

👉Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uzitumie kwenye CV
Usichukue sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.

👉Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. 

Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.

👉Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.

==>Format/Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV:
   1. Lengo la CV na ujuzi wako
    2.Ujuzi wako wa kazi
   3. Mafanikio maalum
   4. Elimu
   5. Ujuzi muhimu binafsi

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Angalizo:
  1.  Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
  2.  Tumia size 9 – 12 ya herufi
  3.   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
  4.   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
  5.   Usitumie sentensi ndefu
  6.  Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha   mafanikio yako kwa uwazi.
  7.  Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma.
   ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 
   ==>.Hakikisha Yafuatayo:
1.Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. 
2.Eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka).  
3.Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu lako kwenye hilo kampuni.
4.Usidanganye

👉Maandalizi ya Mwisho

1.Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
 -Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosea yako.

2.Mpe Rafiki  yako apitie CV
-Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba maelezo yaliyoelezwa humu yatakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kuandika CV safi, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini.

AU 

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.