Skip to main content

FAHAMU WANYAMA 10 WENYE AKILI ZAIDI DUNIANI



Kipimo cha IQ ni njia pekee inayoaminiwa kupima uwezo wa akili za mtu ambapo kwa kawaida binadamu wengi wana IQ ya kuanzia 90 mpaka 110 lakini watu wachache sana wana IQ level ya kuanzia 140 na kuendelea.

Wapo wanyama pia ambao wametambulika kuwa miongoni mwa wanyama wenye akili zaidi duniani kutokana na mienendo yao.

Utafiti uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York Marekani umegundua wanyama wenye akili karibiana na binadamu ambapo utafiti huo ulionesha jinsi gani mazingira wanayoishi yanavyowafanya kuwa wenye akili.

Hawa hapa ndiyo wanyama 10 wenye akili zaidi duniani.

Tembo

Tembo wana akili kubwa kuliko mnyama yeyote wa ardhi kavu, tembo ana uwezo wa kutafuna majani ya dawa kuanzisha uchungu wa kuzaa, kutambua vitu kwenye kioo, kuigiza sauti mbalimbali na kutumia vitu mbalimbali kwa matumizi sahihi pasipo kufundishwa, pia ndiyo wanyama pekee wanaoweka msiba pale mwenzao anapokufa.
Mambo 10 kushangaza usiyoyajua kuhusu Kuku

2. Pweza

Ana uwezo wa kutoroka akikamatwa na kufungiwa kwenye mzingile (maze) ana ubongo mkubwa kuliko wanyama wote wasio na uti wa mgongo lakini pia wana uwezo mkubwa wa kujua maadui, ndio mnyama pekee wa kundi hilo kutumia zana, hujibadili kukwepa maadui, mfano mzuri ni Pweza Paulo aliyetabiri Hispania kuchukua kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Kisa kupoteza Ng’ombe, Baba amuua Mtoto wake

3. Njiwa

Ana uwezo wa kutambua herufi zote 26, ana uwezo wa kurudi nyumbani hata akiwa kilomita mia kutoka nyumbani na ndiyo sababu walikuwa wanatumika kutuma ujumbe kwa wauza madawa ya kulevya pia wanatumika kuuza madawa hasa magerezani.

4. Mbwa

Ni marafiki wakubwa wa binadamu, ambapo mbwa wa kawaida ana akili sawa na mtoto wa binadamu mwenye umri wa miaka miwili, wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu, kujilinda, na kujifunza kutoka kwa binadamu.

5. Panya

Ana uwezo wa kuhesabu, kutambua muda, kuwasiliana na wenzake na kuwa na uhusiano mzuri na binadamu kama anafugwa.

6. Sokwe

Ana uwezo wa kujifunza kutamka baadhi ya maneno kuwasiliana na wenzake kutumia vitu kwa matumizi yake sahihi na huwa anaumia pale mwenzake anakufa.

7. Nguruwe

Wanatunza kumbukumbu kwa muda mrefu, wana uwezo wa kuwasiliana na wenzake na ndiyo mnyama msafi zaidi katika wanyama wanaofugwa.

8. Nyangumi

Ndiyo mnyama mwenye ubongo mkubwa zaidi kama ilivyo Pombo, nyangumi anaweza kuwasiliana na wenzake na kwa sauti mbalimbali na kujifunza pia.

9. Kasuku

Anaweza kujifunza maneno, herufi na namba uwezo wake kiakili unafanana na binadamu wa miaka minne.

10. Pombo

Hawa kwa lugha ya kingereza hufahamika kama Dolphins ni wanyama ambao binadamu huwatumia kutatua matatizo mengi hususan ya baharini. Akili ya pomboo ni kubwa kama miili yao, huonyesha hisia mbalimbali, hujifunza vyema mazingira yao, nusu tu ya akili yake hulala, nusu nyingine ikiwa macho kukabiliana na tishio lolote.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.