Skip to main content

NDANI YA SIKU TATU TANI 37 ZA PWEZA ZAVULIWA SONGO SONGO




Na Ahmad Mmow, Lindi.

Tani 37 na kilo 599 za pweza wenye thamani ya shingi 150,396,000 walivuliwa kwa muda wa  siku tatu baada ya kufunguliwa mwamba laini katika kijiji cha Songosongo,wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.

Hayo yameelezwa na mtendaji wa mradi wa usimamizi wa uvuvi katika wilaya za Mtwara, Kilwa na Kibiti wa shirika la kimataifa la usimamizi na uhifadhi wa mazingira duniani( WWF), Thomas Charles alipozungumza na Muungwana Blog  mjini Kilwa Masoko leo.

Thomas alisema baada ya kufunguliwa mwamba laini uliofungwa katika eneo la bahari ya Hindi lililopo katika kijiji cha Songosongo, pweza wenye uzito watani 37 na kilo 599 zenye thamani ya shilingi 150,396,000 walivuliwa kuanzia tarehe 29. 9.2019 hadi tarehe 1.10.2019.

" Niuvunaji mkubwa ambao haujawahi kufanyika katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Pweza hao niwengi kulinganishwa na muda uliotumika kuvua," alisema Thomas.

Mtendaji huyo alibainisha kwamba tani 23 kati ya tani hizo 37.599 zilinunuliwa na kampuni ya TANPESCA, ambayo ni mmiliki wa kiwanda cha kusindika samaki kilichopo katika wilaya Mafia, mkoa wa Pwani. Huku tani nyingine zilizosalia zilinunuliwa na kampuni nyingine.

Alitoa wito kwa wavuvi wawe waaminifu kwakutoingia nakuvua kwenye maeneo ambayo wananchi wa maeneo hayo wameamua kuyapumzisha kwa muda maalumu yasifanyike shughuli uvuvi. Huku akiwaasa wananchi kutunza na kuhifadhi raslimali za bahari ili yawe na uvunaji endelevu.

Thomas alisema tangu kuanza mpango wa kufunga( kupumzisha) na kufungua mwamba katika katika eneo hilo ni mara ya nne. Ambapo kiasi cha pweza wanaovuliwa kimekuwa kikipanda.

Maeneo mengine ambayo yanapumzisha miamba ni Somanga,Songomnara na  Kivinje katika wilaya ya Kilwa na katika wilaya ya Kibiti ni kijiji cha Pongwe.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.