Skip to main content

KANUNI MUHIMU ZA UFUGAJI WA NG,OMBE WA MAZIWA



Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ni moja kati ya ufugaji unao wakomboa wafugaji wengi sana endapo watazingatia kanuni za ufugaji bora, mimi mwenyewe nimekua shahidi nikiona watu wengi wana piga hatua kutokana na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia sana wakati unataka kuanza na hata kama umeanza kufuga ng'ombe wa maziwa;

Uchaguzi wa aina bora ya ng'ombe
Hili ni jambo la msingi sana kabla ya kuanza kufuga unatakiwa ujue je ni aina gani ya ng'ombe bora ambaye anaweza kunifaa .

Lakini kwa ufupi kuna aina tano kubwa ambazo zinatumika sana
Fresian
Guersey
Jersey
Ayrshire
Brown swiss

Hivyo unaweza fanya uchaguzi wako kulingana na mahitaji yako kwa kua kila aina ina sifa tofauti na nyezake japo kua fresian ndio aina inayopendwa sana na ndio aina ambayo inatoa maziwa mengi sana kuliko aina zingine zilizo bakia.

Ujenzi wa banda
Wafugaji wengi hua wamezoe kufuga ng'ombe kienyeji ndo maana wanakua hawapati kulingana na jinsi walivyo tarajia. Banda ni lazima liwe bora ili kuongeza uzalishaji

Banda unaweza kuweka  zege chini ili kuwezesha usafi na pia hii inapunguza magonjwa mengi kama vile kuoza kwa kwato.

Pia banda la ng'ombe wa maziwa unatakiwa kuweka paa juu ili kuzuia mvua na jua kufukia moja kwa moja kwa ng,ombe na hii pia inapunguza maamukizi ya magonjwa pamoja na stress kwa ng,ombe.

Lazima banda bora liwe na mifereji ambayo itasaidia kutoa uchafu nje ya banda wakati wa kusafisha hii itasaidia kuounguza uchafu ndani ya banda.

Madilisha pia yanatakiwa kua makubwa kuwezesha hewa na mwanga wa kutosha kuingia ndani ya banda.

Sehemu ya kulia chakula na pamoja na sehemU ya kunywea maji ni lazima ziwepo.

Kitu kingine lazima sehemu ya kukamulia maziwa iwepo ili iwe rahisi wakati wa kukamua maziwa

Pia ndama lazima walazwe sehemu tofauti na ng'ombe wakubwa.

Chakula
Ili ng'ombe aweze kutoa maziwa ya kutosha ni lazima apewe maji safi na chakula bora na pia lazima  chakula kiwe cha kutosha. kabla ya kuanza kufuga lazima ujiahakikishie chakula cha kutosha na chakukidhi mwanzo hadi mwisho.

Watu wenye eneo hua wanapanda majani ili kuahikisha chakula hakikosekani(pasture). Pia unaweza kukata majani wakati wa masika na kuyatunza vizuri ili kuwalisha wakati wa kiangazi pale malisho yanapokua ya shida.

Pia ng'ombe wa maziwa ni lazima apewe chakula maalumu ambacho kinaongeza maziwa kila siku na hua wanapewa kilo 1 hadi 3 kulingana na uzito wake asubuhi na jioni. n

Pia unaweza kumlisha mapumba au mashudu mabaki ya mazao kama viazi mahindi pia pale majani yanapo kua shida.

Muhimu
Natumaini umejifunza kitu kutoka mwanzo mpaka hapa tulipo fikia, japo kua ufugaji wa ng'ombe sio mgumu sana lakini kunavitu muhimu ambavyo nilazima wewe kama mfugaji uvizingatie ili kuongeza uzalishaji

Ng'ombe ni lazima waoshwe kwa dawa ili kupunguza kushambuliwa na wadudu ambao wanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa kama ECF, na unaweza kuwaosha ng'ombe kila wiki kutokana na ratiba yako pia unaweza kutumia dawa kama TICK FIX, PARANEX  na zingine nyingi.

Lazima banda liwe safi ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kama FOOT ROUT  na usafi unaweza kufanyika kila siku asubuhi au jion.

Ng'ombe lazima apewe chakula na maji safi  ili kuongeza uzalishaji

Pia ni lazima kuwatibu au kuchukua hatua pale ng'ombe anapoonekana kua na ugonjwa ili kuepusha maambukizi kwa wengine na pia ili kumuokoa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.