Watumiaji wa Android wamepewa orodha ya apps za kuziondoa kwenye simu zao kwa sababu za kiusalama wa data na kuondoa matangazo yanayotokea sehemu zisizohusika kwenye simu zao. Ushauri huo umetolewa na watafiti kutoka ESET ambao wamegundua app 42 kwenye soko la Google Play Store ambazo zimekuwa zinakuja na mfumo wa kimatangazo usio rasmi – adware. Mfumo huo una sababisha betri ya simu kuisha haraka, utumiaji wa data – intaneti na ata kuchukua taarifa zako binafsi kwenye simu. Baada ya utafiti wa ESET kuweka wazi Google waliondoa apps hizo kwenye soko lao la Apps, ila inakuitaji wewe kuziondoa mwenyewe. Pia kuzifahamu ni muhimu kwa watu ambao wanatumia masoko mengine ya apps nje ya soko la Google Play Store. Apps hizo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 8. Apps hizo zinauwezo wa kuonesha matangazo ata kama simu imefungwa (locked) kitu ambacho huwa kinapigwa na Google, kwani kufanya hivyo kuna sababisha utumiaji mkubwa wa betri na nje ya makubaliano yao na watengenezaji wa
The main aim of students forums blog to provide the fact and accurate information concerning with students in order to be aware.