Skip to main content

NACTE YAONGEZA MUDA WA UDAHILI WA VYUO KWA MWAKA MPYA WA MASOMO



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Balaza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuongeza muda wa udahili kwa waombaji mafunzo kwa ngazi ya Cheti na Diploma kwa kufungua dirisha dogo la udahili kwa lengo la kuwapa nafasi wale ambao hawakupata nafasi katika udahili wa kwanza au kukosea chaguzi wanazostahili.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dkt Leonard Akwilapo, amesema wameamua kuongeza mda wa udahili kwa sababu wanatambua kuna idani kubwa ya waombaji hawakupata nafasi na wengine walikosa sifa kwa kozi husika waliyoiomba.

“Wizara imeagiza balaza la taifa la elimu ya ufundi (NACTE) kufungua dirisha dogo la udahili kuanzia tarehe 7 mpaka tarehe 21 Septemba, 2019,  ili kujaza nafasi zilizo kwenye vyuo na taasisi mbalimbali za mafunzo za serikali na binafsi  katika kada mbalimbali ambazo zina nafasi ya udahili” amesema Dkt Akwilapo.

Aidha amesema Wizara inatoa rai kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita,  na wale wote waliokosa sifa za kujiunga na mafunzo mbalimbalikutumia fulsa hiyo kufanya maombi ya udahili upya, waombaji  wametakiwa  kuwa makini ili wasije kukosa nafasi ya kujiunga na mwaka wa masomo kwa mwaka 2019/2020.

Aidha amebainisha kuwa kwa waombaji wa kozi ya ualimu kwa  ngazi za  cheti na Diploma udahili ulianza tarehe 3 mwezi wa saba hadi tarehe 30 mwezi wa Nane, 2019, waombaji walielekezwa walielekezwa kuomba kupitia tuvuti ya NACTE kwa waombaji wa vyuo vya serikali na vyuo binafsi walielekezwa kuomba moja kwa moja vyuo wanavyotaka.

“Lakini hadi mwisho wa tarehe ya udahili, waomba walikuwa 7,025 waliokamilisha maombi yao, na waliokidhivigezo walikuwa 5,252(75%) na 1,773(25%) hawakuwa na sifa zinazotakiwa kujiunga na mafunzo ya ualimu,  wakati nafasi zilikuwa 12,859 katika vyuo 35 vinavyotoa mafunzo hayo,” amesema.

Pia amebainisha jumla ya waombaji 11,028, walichaguliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) na NACTE na kupangiwa vyuo vya mafunzo ya ualimu na majina yao yanapatikana kwenye  tuvuti ya  ya Wizara na NACTE.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha udahili wa NACTE, Twaha Twaha, amewatahadharisha waombaji hasa wa kitengo cha Nessing na Clinical Medicine lazima wawe na ufaulu katika masomo  ya Physics, Chemistry na Biology lazima vizingatiwe katika maombi.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.