Skip to main content

MBINU ZA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA KAZI NA MAISHA KWA UJUMLA




Zifuatazo ni njia kila mtu haswa viongozi waweza zitumia kuongeza ubunifu binafsi na wa wale wwanaofanya nao kazi;

Tengeneza mazingira na mbinu ya kufanyia kazi mawazo yako ya kibunifu na yale ya wale unaofanya nao kazi.

Kuwa na mawazo ya kibunifu ni jambo jema lakini kuishia kua na mawazo ya kibunifu ni kazibure, ni lazima kazi ya ziada ifanyike ya kutengenenza mazingira kwa ajili ya kuanza fanyiakazi hayo mawazo ya kibunifu yaliyopatikana, unapokua umefanya uchunguzi yakinifu juu ya uwezekano wa kufanikiwa na kiutendaji wa wazo bunifu ni muhimu sana kuamua kuanza wekeza muda na rasirimali katika kuanza kulitendea kazi wazo hilo la kibunifu . Pale watu unaofanya nao kazi wanaona mawazo yao ya kibunifu yanafanyiwa kazi itawapa hamasa zaidi ya kuzidi kua wabunifu zaidi na hii huchipua ufanisi katika kazi.

Fanya maamuzi kwa kushirkishana na kuulizana na si kuamrishana
Watu wengi walio wabunifu hawapendi kuamrishwa sana, hupenda kufanya vitu kufuatia kusudio na kwa ridhaa ya mioyo yao. Na katika mazingira ya kazi hii lazima ianze kuwa tabia ya viongozi haswa wa juu na kama kiongozi ni muhimu sana kuwahamasisha uwaongozao kujenga tabia ya kutokuamrishana bali kuelekezana majukumu kwa njia ya kistaarabu issyo mfanya mwingine kujihisi kunyimwa uhuru wa kuchagua na kuamua na waonapo wewe kiongozi wajuu unaishi taratibu hiyo mpya hata wao watavutika kuiishi na hata kupelekea ubunifu kuongezeka na hivyo ufanisi.

Jenga misingi ya kuaminiana na kuheshimiana baina ya viongozi wakubwa na wafanyakazi wa kawaida.

Mawazo bora ya kibunifu huweza tokea kutoka kwa mtu yeyote pasipo kuzingatia hali yake, elimu yake ma cheo chake, hivyo ni muhimu misingi ya kuheshimiana na kuaminiana ikajengeka ili kuruhusu wafanyakazi wote kua huru kuelezea mawazo yao katika hali ya kujiamini mbele ya watu wote na kuyafanyia kazi yote pasipo ubaguzi kwani hii itachangia ushirikiano na kujenga hali ya kujiamini na kujaribu zaidi hata kuchipua uwezo wa kibunifu ndani ya wafanyakazi wote ,hii huleta ufanisi katika kazi.

Futa tamaduni ya kushindikana kwa mawazo
Watu wengi sana ubunifu wa mawazo yao umepotea hivi hivi kutokana na hali ya kujiaminisha kua mawazo yao hayawezekani kwa sababu wanazoziiita zipo nje ya uwezo wao, hivyo ile hofu ya kushindikana kwa mawazo kumepelekea kuua uwezo wa kibunifu wa watu wengi, na hii inadhihirika katika kuogopa maneno ya watu wengine ikiwemo kebehi, dharau na vicheko. Na njia pekee ya kuiiondoa hii tamaduni ni kuwajenea wafanyakazi wako uhakika wa kufaulu na kushindwa kwa mawazo yao na kuwahakikisha wote wanaelewa mchango wa kushindwa katika kuja na mawazo bora zaidi ya kibunifu, Kushindwa ni moja ya njia muhimu sana kuanzisha na kuendesha biashara yeyote na kila kushindwa huleta mafunzo muhimu sana ambayo huchangia kuongeza ufanisi katika kazi.

Teneneza mazingira ambayo mawazo yaliyoshindwa hayatazungumziwa katika vikao vya thathmini vya kikazi ama kuhuishwa katika utoaji wa fidia na kuishi na tamaduni kua njia pekee ya kua mbunifu zaidi ni kushindwa zaidi na kutafuta namna ya kuboresha utendaji wa pale paliposhindikana kwani hata watu wabunifu sana hukosea mara nyingi tu.

Hivyo kumbuka kua ni kupitia ubunifu pekee ukuaji wa biashara na maendeleo huja na kupitia ubunifu pekee ufanisi

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.