Skip to main content

KANUNI ZA KUFANYA KILIMO BORA



Kwa kilimo chochote kile ambacho unatamani sana kukifanya zipo kanuni na taratibu zake za kuweza kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya msingi ambayo ni muhimu kuweza kufanya hivyo ni pamoja na;

Kutayarisha shamba mapema
Shamba ni lazima litayarishwe mapema. Matayarisho hayo ni pamoja na kufyeka, kukwatua na kulima.

Kutumia mbolea: 
SAMADI: Ihamishiwe shambani mapema kabla ya mvua kuanza.
MBOLEA ZA VIWANDANI: Tumia mbolea za kupandia kama vile Minjingu Rock Phosphate (MRP), DAP na NPK. Zikifuatiwa na za kukuzia kama UREA na CAN.

Upanda  mapema
Panda mara mvua za kwanza zinapoanza kunyesha.

Kutayarisha mbegu bora mapema
Nunua mbegu au tayarisha mbegu nzuri kutokana na mavuno yaliyopita kama ulitumia mbegu mchanganyiko.

Mbegu chotara (hybrid) zisirudiwe. Mbegu bora ziwe zilizopendekezwa kwenye ukanda/eneo lako.

Panda kwa nafasi zinazotakiwa
Hakikisha umepanda kila zao kwa nafasi maalum inayoshauriwa kitaalam. Rudishia mapema pale ambapo mbegu hazikuota.

Kupalilia vizuri na kwa wakati
Hakikisha shamba lako halina magugu wakati wote kwa kupalilia mapema. Wakati wa kupalilia punguzia miche na kuinulia matuta.

Kudhibiti magonjwa, wadudu na ndege waharibifu wa mazao
Tumia njia za kitaalam za kudhibiti magonjwa, wadudu na ndege waharibifu wa mazao.

Kuvuna mapema
Vuna mazao yako mapema mara yanapokomaa na kukauka vizuri. Vuna kwa wakati ili kuepuka mazao yako yasiharibike kwa jua, mvua na wadudu.

Kuhifadhi mazao vizuri
Mara baada ya kuvuna na kukausha mazao vyema, hifadhi kwenye vyombo vya kuhifadhia kama vile vihenge na magunia. Hakikisha umeweka dawa za kudhibiti wadudu waharibifu.

Kusafisha shamba mapema baada ya kuvuna.
Ng'oa mabua na masalia ya mazao na kuyalaza kati ya matuta na kuyafunika kwa udongo ili yaoze mapema. Kwa mazao ya tumbaku na pamba ng'oa na kuchoma moto mabua yake mapema.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.