Skip to main content

ZIJUE SABABU YA MALENGO MENGI KUTOKUTIMIA.



Moja yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio yake yanatimia, hata hivyo kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo.

Ipo hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali fulani, moja ya maada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana na jinsi gani unavyoweza kutimiza  malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhairi anayo ndoto ambayo inasukuma kufikia kilele cha mafanikio.

Ndipo nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini ambacho anaadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwake. Baada ya kumaliza zoezi hilo la kujua kila mtu lengo lake, ndipo nikawataka watu hao hao waandike kuhusiana na njia ya kutimiza ndoto hizo.

Moja ya maajabu ambayo niliyaaona ni kwamaba watu wengi ni wazuri sana wa kusema nataka kuwa mtu fulani lakini linapokuja suala la utekelezaji wa jambo hilo hapo ndipo ukakasi hujitokeza unajua ni kwanini? Niligungundua ya kwamba watu wengi wana ndoto lakini hawajui mbinu za kutekekeza, hata wale ambao wanajua ni wepesi sana wa kukuta tama. Ndipo nikawambia ya kwamba kwa jambo lolote ambalo unalitamani liwe kweli ni lazima ujue mbinu ya utekelezaji wa jambo hilo hususani kwa kujifunza na ikiwezekana kulipa gharama lipa gharama kwa kuwa hakuna maisha ya kimafanikio ambayo hayana gharama.

Pia ikubukwe ya kwamba katika kujifunza hukohuko kuna changamoto zake, changamoto hizo hizo ndizo ambazo huwafanya watu wachache waweze kuhimili mikiki ya  jambo hilo, na hawa ni watu ambao wamefanikiwa katika sayari hii. Hata hivyo kwa asilimia kubwa ambapo wengi wetu ambao ndio tupo humo huwa hatupo tayari kuvumilia mikikimikiki ya changamato ambazo mara nyingi hujitokeza katika mambo amabayo tuanayafanya.

Wengi wetu tupo tayari kuhairisha mambo  na kuleta visingizio visivyokuwa na maana yeyote ile, kwa mfano unakutana na mtu anakwambia anataka kufanya biashara fulani lakini changamoto yake kubwa ni  mataji. Kimsingi ukichunguza changamoto hiyo utagundua ya kwamba ni sababu yatima, nikiwa na maana ya kwamba huna haja ya kuacha kufanya jambo fulani eti kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.

Tuende mbele turudi nyuma na kuyatafakari maisha ambayo tunayaishi leo hii, ni kwanini yapo vile vile? Ni wakati wako muafaka ewe msomaji ambaye unasoma makala haya kuweza kutafakari kwa umakini jambo hili japo kwa dakika chache na kuendelea kutafakari juu ya maisha yako. Tafakari ni kwanini mapka leo hii hujatimiza malengo yako? Kama umepata jibu zama tena katika halmashauri yako ya kichwa tafakari tena je unahisi sababu ambazo umezipata ni za msingi au  sio za msingi? Kama umekwisha pata majibu inua macho yako mbiguni, tazama mbigu inavyong`ara kisha tafakari tena na uje na majibu ya kina je unachukua hatua gani kwa hayo yote uliyowaza? Usinibe majibu.

Mmmh, sawa labda nisiendelee kuongea sana, maana naweza nikakupoteza kabisa ila cha msingi ni kwamba tafakari hayo machache kisha uchukue hatua mathubuti za kiutendaji. Hata hivyo nikazie kwa kusema ya kwamba mara zote ukiwa na malengo usiishie kusema tu, bali onyesha njia sahihi za utekezaji. Kufanya hivi kutukupa mwelekeo tosha kwa upande wako kwa kuonesha ni nini! Ambacho unatakiwa kuwa nacho? Na baada ya muda gani!

Huenda bado ukawa haujanielewa nazungumzia masuala ya uwezo wa utekelezaji wa jambo hilo. Maana tunafahamu ya kwamba ili yaitwe mafanikio kuna njia ya kufikia mafanikio hayo kwa mfano kujifunza kutoka kwenye vitabu, video, semina na watu wengine ambao kiujumla wamekwisha fanikiwa. Nikakumbushe kwa mala nyingine kuwa ni lazima uwe na picha kamili ya kule ambapo unataka kuelekea.

Nikushuru sana kwa kusoma makala haya, lakini shukrani zangu zangu zitakuwa zimekamilika endapo utachukua hatua kwa hayo ambayo umekwisha yasoma kwenye makala haya. Nikusihi ya kwamba ulichojifunza mshirikishe mwenzako kama ambavyo mimi nmefanya kwako.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.

NAFASI 37 ZA KAZI TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) DEADLINE 29/11/2019

The Tanzania Institute of Accountancy (TIA) is an Executive Agency under the Ministry of Finance and Planning which was established on 1st July, 2002 by the Government Notice No. 489 of 1st November, 2001 and officially launched on 24th January, 2002 as per Act No. 30 of 1997. As an Executive Agency, TIA is operating ‘semi’ autonomously and commercially in providing quality education in the field of Accountancy, Procurement & Supplies and other Business related disciplines so as to become a self-sustainable Institute. TIA is accredited by NACTE as an Institute of Higher Learning Education. ==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi ; << Ingia Ha>> The Institute is looking for qualified and dedicated personnel to fill the post of Tutorial Assistants on contract basis. The table below provides details on a particular fields/ professionals one should apply against. ==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi ; << Ingia Ha>>