Skip to main content

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA NOTI BANDIA



Mkazi wa Magomeni Mapipa Mariam Zuberi (21), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kukutwa na noti 20 za bandia.

Akisomewa hati ya shtaka mbele ya Hakimu Lilian Silayo na mwendesha Mashtaka wa Serikali Ester Charles amedai mnamo Juni 27, 2019 eneo la Magomeni Wilaya ya  Kinondoni, Dar es  Salaam bila kuwa na idhini ya mamlaka husika, alikutwa na noti 20 za bandia za sh 10,000 zenye thamani ya Sh 200,000.

Noti hizo zina namba  za usajili GF4658564  noti 5, GF4658572 noti 4, GF4658567 noti 3, GF4658561 noti 2, GF4658562 noti 2, GF4658563 noti 1 na BK8169395 noti 1 huku akifahamu kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo mbele ya mahakama, huku upande wa Jamuhuri ukisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na  kuomba tarehe ya kesi kusikilizwa tena.

Hakimu Silayo amesema fungu la dhamana liko wazi kwa masharti kwa kuwa na  wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi zinazo tambulika kisheria na nakala ya vitambulisho vinavyotambulika na serikali ambao watasaini bondi ya Sh 500,000 kwa kila mdhamini.

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa mpaka kesi yake itakaposikilizwa tena Septemba 26 Mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.