Skip to main content

CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU MOMBA YAATHIRI WANAFUNZI WA CHUO CHA DIT




Halmashauri ya wilaya ya Momba  mkoani Songwe inakumbwa na changamoto ya mitandao ya simu muda mrefu jambo ambalo limeonekana kuwa ni kikwazo kwa wanafunzi wa chuo cha  Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Slaam (DIT) Kampasi ya Myunga Momba  kujifunza na kwendana na kasi ya maendeleo ya teknolijia Duniani.

Chuo cha Taasisi ya Teknolojia ya Dareslaam (DIT) Kampus ya Myunga ni chuo cha kwanza cha serikali mkoani Songwe ambacho kinategemewa kutatua changamoto mbali za ukosefu wa watalaam upande wa ufundi sanifu, sayansi na uhandisi katika fani mbalimbali.

wadau  wanafunzi  pamoja na wameilezea changamoto hiyo ya mawasiliano katika hafla ya awamu ya kwanza ya mafunzo ya udereva yaliyoendeshwa na chuo cha VETA Mbeya wakishirikiana na DIT Kampasi ya Myunga .

Dk Frenk Lujaji Mkurugenzi wa Chuo cha DIT Kampasi ya Miyunga alisema kuwa mtandao ni muhimu sana kwa chuo hicho kwa kuwa kimejikita zaidi katika ufundi ambao unaendana sambamba na teknolia ambayo inakua kila siku kutokana na maendeleo ya Sayansi Duniani kwa ujumla.

"Sisi kama chuo baada ya kuona chanagamoto hii ni kubwa tuliamua kuwasiliana na TTCL ambapo wanaendelea kutuboreshea ili tuweze kwendana na teknolojia, kila kitu unacho fanya katika teknolojia lazima ufanye ulinganifu na sehemu zingine Duniani, hivyo kupatikana kwa mtandao wa uhakika kutaboresha mawasiliano na kuboresha mafunzo kwa wanafunzi ili kwendana na Soko la ajira na kujiajir" alisema Dk Lujaji.

Aliongeza kuwa lengo la chuo hicho ni kuukwamua mkoa wa Songwe kiuchumi, kwa kuzalisha mafundi na watalaam mbalimbali wano hitajika katika soko la ajira .

Adam Zakaria Kinyekile Injinia wa mitaani ambaye anatengeza ajira kwa mafundi mbalimbali kutoka vyuo vikuu nchini kutokana na ubunifu na uzopefu wake katika fani hiyo alisema kuwa katika ufundi mitandao ya simu na Internet ni muhimu sana ili kuweza kutengeneza vitu vyenye ubora kulingana na soko la Dunia linavo hitaji'

Pia ameitaka serikali kuwatambua mafundi wa mitaani walio na vipaji na uzoefu mkubwa katika fani hiyo ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiserikali kama wazawa.

"Mitaani tupo mafundi wazuri sana ambapo tukitumiwa na serikali bila kujali kuanagalia cheti twaweza kunufaika na kunufaisha nchi yetu , mimi wanafunzi wengi kutoka vyuo vikuu huja kufanya mazoezi kwa vitendo kwangu na nmefundisha watu wengi sana ambao tayari walishajiajiri na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana" alisema Kinyekile.

Godfrey Siame Diwani wa Kata ya Ikana eneo kilipo chuo hicho alisema changamoto ya mitandao ni changamoto kwa wananchi wake hata eneo zima la wilaya ya Momba jambo ambalo hupelekea mawasiliano kuwa magumu na kukwamisha baadhi ya shughuli muhimu hata za Kiserikali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe John Palingo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo alisema kuwa tayar mkoa umesha orodhesha maeneo yote ndani ya mkoa ambayo yanachangamoto mitandao ili kufanyiwa kazi na wizara husika.

"Hii changamoto ya mitandao itaisha mwaka huu wa fedha kwa sababu tayari tumeshaainisha maeneo yote na tayari kwa kukupeleka Tamisemi ili kufanyiwa kazi kufanyiwa kazi " alisema Palingo.

Aidha Palingo alikitaka chuo hicho kujikita kutoa elimu iliyo bora na yenye ushindani ili kushindana na nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo nchi 16 zilizo kusini mwa Afrika (SADC)

"Ajira zitakuwa wazi kwa nchi zote wanachama hivyo tutotoe elimu bora yenye kukidhi mahitaji ya nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo nchi 16 zilizo kusini mwa Afrika (SADC), tuanzishe programu za uzalishaji bidhaa kwenye kilimo ambazo uhitaji wake ni mkubwa" alisema Palingo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.