Skip to main content

TEKNOLOGIA KUMI(10) ZILIZOVUMBULIWA NA WANAWAKE



Mara nyingi michango ya wanawake katika sekta muhimu kama Teknolojia na sayansi haionekani lakini historia inaonesha jinsi gani wanawake walivyotoa mchango mkubwa hasa katika karne ya mapinduzi ya viwanda.

Leo nimeona nikuletee hii listi ya wanawake waliotoa mchango mkubwa katika kufanya vumbuzi mbalimbali za kisayansi duniani.

1:Florence Parpart.
Mwaka 1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme ambapo uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia baada ya kuvumbuliwa na mwanamke.

2:Marie Van Brittan.
Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera ya cctv mwaka 1969,,ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika jiji la Newyork.

3: Stephanie Kwolek .
Stephanie Kwolek atakumbukwa kwa uvumbuzi wake wa material iliyotumika kutengeneza bullet proof.

4:Hedy Lamarr’s .
Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua teknolojia ya wireless iliyo saidia kuanzishwa kwa wiFi na mfumo wa GPS.

5:Josephene Cochrane.
Mwaka 1887 Josephene Cochrane alivumbua machine ya kuoshea vyombo au dish washer ambazo alikua akiziuza mahotelini mwaka mmoja baadae alifungua kiwanda chake.

6:Letitia Gee.
Mwaka 1899 Letitia Geer Alivumbua bomba la sindano na kubadilisha historia ya sekta ya afya milele.

7: Dr Maria Telkes.
Dr Maria Telkes mwaka 1947 alijenga nyumba ya kwanza duniani yenye mfumo wa umeme wa jua au solar energy.

8:Maria Beasely.
Mwaka 1886 Maria Beasely alibuni maboya ya kuogelea au life jackets baada ya kukithiri vifo vya baharini , ni uvumbuzi uliopongezwa na watu wengi na kumfanya Maria Beasely kua mwanasayansi mwenye jina kubwa.

9:Dr Shirley Jackson
Ni mwanafizikia aliebuni nyaya au fiber cable zinazotomika leo hii kwenye mitandao ya simu, pia uvumbuzi wake mwingine ulio mjengea jina ni pamoja na machine ya fax, mfumo wa kusubirisha mtu kwenye simu au call waiting.

10:Ada Lovelace.
Unaweza usiamini lakini computer programmer wa kwanza kabisa duniani ni mwanamke ,Ada Lovelace alikua mtu wa kwanza kubuni program mbalimbali za computer.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUWA MWANDISHI MZURI WA VITABU

Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu  zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...

HEKA HEKA VIWANJANI;KIKOSI CHA TIMU YA HR\MKT WAFANIKIWA PENYA NUSU FAINALI BAADA YA KUWACHAPA MECHANICS KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT).

Hiki ndicho kikosi cha timu ya HR\MKT kilicho wachabanga MECHANICS Kwa goli moja bila katika kipindi cha kwanza goli lilofungwa na mchezaji mahiri maarufu kama (Jay) mwenye jezi nambari 17 mgongoni ni James Philimon akiwa na magoli matano katika michuano ya interclass na hadi kipenga cha mwisho muamuzi wa mchezo huo kumaliza mchezo na kuwafanya HR\MKT chukua point tatu muhimu mbele ya washika spana MECHANICS na kujikusanyia point tisa(9) na kufanikiwa kuingia nusu fainali Matokeo yakiwa HR\MKT 1 na MECHANICS O Hichi ndicho kikosi cha MECHANICS kilicho shindwa kutamba mbele ya timu ya mafisa waajiri wakiungana na mafisa masoko na kufanikiwa kuwatoa katika michuano ya interclass inayoendelea katika chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI TANZANIA (NIT) KINACHO TOA MAFUNZO MBALI MBALI YA USAFIRISHAJI KINAHAKIKISHA SETKA YA UCHUKUZI INAKUWA IMARA SIKU BAADA YA SIKU.