Moja yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio yake yanatimia, hata hivyo kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo. Ipo hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali fulani, moja ya maada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana na jinsi gani unavyoweza kutimiza malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhairi anayo ndoto ambayo inasukuma kufikia kilele cha mafanikio. Ndipo nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini ambacho anaadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwak