Leo mida ya alaasiri miamba miwili ilipimana nguvu baina ya timu ya IT\COMP.SC VS MECHANICS mpaka kuelekea mapumziko timu ya IT\COMP.SC ilifanikiwa kwa kuongoza goli moja bila na lilofungwa na mchezaji mahiri aliye valia jezi nambari 20 mgongoni mwake.baada ya mapumziko dakika kadha wataalamu wa ufundi(MECHANICS) waka sawazisha goli kupitia mchezaji wao machachari aliye valia jezi nambari 12 na kuwafanya watalamu wa sayansi ya mawasiliano(IT COMP.SC) Kubaki midomo wazi na mpira kumalizika kwa kutoka suluhu ya moja moja.IT\COMP.SC 1 na MECHANICS 1
Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chagua mada ambayo inahitajiwa na wasomaji. Chagua mada ambayo haikiuki sheria au maadili ya eneo unalolenga. Chagua mada ambayo inaziba pengo lililoachwa na vitabu vingine. 2. Pangilia kabla ya kuandika Mpangilio ni...
Comments
Post a Comment
Yes